Latest Updates

HUZUNI IKIZIDI FURAHA NI MUDA MWAFAKA WA KUVUNJA MAPENZI: JASON DA RULO

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa RNB na POP kutoka nchini Marekani JASON DE RULO ameweka wazi kuwa sababu kuu ya kuvunjika kwa mahusiano kati yake na mwanamziki JORDAN SPARKS ni kukithiri kwa mafarakano kati ya wapenzi hao wawili. JASON alifunguka kuhusiana na kuvunjika kwa mahusiano yao katika mazungumzo na Ryan Seacreth ambapo Jason alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyochochea kukosekana kwa amani ya mahusiano kati ya wawili hao ni pamoja na shinikizo la ndoa kati yao na mwanadada huyo JORDAN SPARK. awali kuvunjika kwa mahusiano kati ya wawili hao kulileta taharuki kubwa hususani ni miongoni mwa mashabiki na watu waliokuwa wakifuatilia mahusiano wanamziki hawa kwani awali haikuwahi kuripotiwa habari yoyote ya mafarakano baina ya wapenzi hawa. Katika mazungumzo na ryan Seacreth De Rulo alikiri kuwa kuvunjika kwa mahusiano hayo haikuwa kwa uzuri lakinhakuna chuki yoyote inayoendelea kati yao kwani wameachana kwa amani njema na sio shari kama ilivyokuwa kwa copules wengine.

0 Response to "HUZUNI IKIZIDI FURAHA NI MUDA MWAFAKA WA KUVUNJA MAPENZI: JASON DA RULO"

Post a Comment