Latest Updates

JE MIKE TEE ANAPANDA AU KISHUKA? mashabiki wahoji

ni wiki chache sasa zimepita baada ya nguli wa mziki wa kizazikipya MIKE TEE A.K.A Mnyalu kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la kiduchu. wimbo huu umepokelewa kwa mtazamo tofauti miongoni mwa mashabiki wake kutokana na mtindo alioutumia Mike Tee kwenye kibao hiki.
    mapema wiki hii mwandishi wa blogu yetu alitembelea mitaa ya TEMEKE mwembe yanga ambapo alishuhudia ubishani mkubwa baina ya mashabiki wa mwanamuziki Mike Tee wakibishani kuhusu ubora wa muziki wa msanii huyu kwa sasa.
mmoja wa mashabiki hao ambae jina lake limehifadhiwa alidaikuwa yeye binafsi hapingi mtindo wa muziki ufanywao na Mike Tee kwa sasa lakini aridhishwi na ufanisi wake pia.
shabiki huyu alielezea kuwa utendaji wa sasa wa MIKE TEE utamgharimu kuwapoteza washabiki wake wa zamani na kuanza kutengeneza hadhira mpya suala ambalo litamgharimu fedha na muda pia.
kwa upande wa Shabiki mwingine  alitetea kuhusu mabadiliko ya sanaa ya  Mike Tee akieleza kuwa soko la muziki Tanzania limekua na pia linapokea mabadiliko kila siku suala ambalo pia wasanii wanapaswa kuzingatia ilikukidhi haja za burudani kwa Mashabiki wao.
kwa upande wake anayatazama mabadiliko ya mwanamuziki huyu katika mtazamo chanya na kuongeza kuwa kila mtu anafikra na mtazamo tofauti hivyo kiasi kinahitajika kwa wanasanaa ilikukidhi matakwa ya mashabiki wao,ambao pia wamegawanyika katika matabaka tofauti.