Latest Updates

HIVI NDIVYO ILIKUWA MAVOCO ALIPOTAKIWA KUSHOOT VIDEO KARIBU NA MNYAMA CHEETAH

Ni baada ya watanzania wengi kupongeza juu ya ubunifu na uzuri wa video mpya ya wimbo wa msanii Richard Mavoco ulioshutiwa huko capetown Afrika ya kusini ambapo ndani ya wimbo huo msanii Richard mavoco anaonekana akiimba karibu kabisa na mnyama wa porini aina ya cheetah, msanii huyo amefunguka juu ya vile alivyopatwa uwoga wakati wa zoezi zima la kupiga picha na cheetah" "Nakumbuka wakati tumefika pale hali ilibadirika ghafla cause mpango ulikuwa ni kwamba Cheetah apigwe shot za peke yake akiwa anatenbea,lakini Adam akabadilisha script akasema Mavoco inabidi uimbe na Cheetah,mwanzo niligoma kabissa lakini kwa ushawishi wa yule mama anayemfuga na Adam ikajikuta nimekubali.

HUZUNI IKIZIDI FURAHA NI MUDA MWAFAKA WA KUVUNJA MAPENZI: JASON DA RULO

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa RNB na POP kutoka nchini Marekani JASON DE RULO ameweka wazi kuwa sababu kuu ya kuvunjika kwa mahusiano kati yake na mwanamziki JORDAN SPARKS ni kukithiri kwa mafarakano kati ya wapenzi hao wawili. JASON alifunguka kuhusiana na kuvunjika kwa mahusiano yao katika mazungumzo na Ryan Seacreth ambapo Jason alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyochochea kukosekana kwa amani ya mahusiano kati ya wawili hao ni pamoja na shinikizo la ndoa kati yao na mwanadada huyo JORDAN SPARK. awali kuvunjika kwa mahusiano kati ya wawili hao kulileta taharuki kubwa hususani ni miongoni mwa mashabiki na watu waliokuwa wakifuatilia mahusiano wanamziki hawa kwani awali haikuwahi kuripotiwa habari yoyote ya mafarakano baina ya wapenzi hawa. Katika mazungumzo na ryan Seacreth De Rulo alikiri kuwa kuvunjika kwa mahusiano hayo haikuwa kwa uzuri lakinhakuna chuki yoyote inayoendelea kati yao kwani wameachana kwa amani njema na sio shari kama ilivyokuwa kwa copules wengine.

JAYZ- AJISOGEZA UGANDA

Rapper na mwanamuziki nguli wa mziki wa hiphop nchini Marekani JAYZ ameripotiwa na chombo cha habari cha THE INSIDER kuwa amefungua tawi la club yake almaarufu kama CLUB 40/40 katika jiji la kampala nchini Uganda. the Insider imeripoti kuwa CLUB 40/40 iliyopo nchini humo itakuwa ni tawi la kwanza kabisa nchini Afrika la CLUB YA 40/40 ambayo kwa sasa imekuwa na umaarufu mkubwa miongoni mwa wasanii na watu maarufu nchini Marekani