Latest Updates

JE MIKE TEE ANAPANDA AU KISHUKA? mashabiki wahoji

ni wiki chache sasa zimepita baada ya nguli wa mziki wa kizazikipya MIKE TEE A.K.A Mnyalu kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la kiduchu. wimbo huu umepokelewa kwa mtazamo tofauti miongoni mwa mashabiki wake kutokana na mtindo alioutumia Mike Tee kwenye kibao hiki.
    mapema wiki hii mwandishi wa blogu yetu alitembelea mitaa ya TEMEKE mwembe yanga ambapo alishuhudia ubishani mkubwa baina ya mashabiki wa mwanamuziki Mike Tee wakibishani kuhusu ubora wa muziki wa msanii huyu kwa sasa.
mmoja wa mashabiki hao ambae jina lake limehifadhiwa alidaikuwa yeye binafsi hapingi mtindo wa muziki ufanywao na Mike Tee kwa sasa lakini aridhishwi na ufanisi wake pia.
shabiki huyu alielezea kuwa utendaji wa sasa wa MIKE TEE utamgharimu kuwapoteza washabiki wake wa zamani na kuanza kutengeneza hadhira mpya suala ambalo litamgharimu fedha na muda pia.
kwa upande wa Shabiki mwingine  alitetea kuhusu mabadiliko ya sanaa ya  Mike Tee akieleza kuwa soko la muziki Tanzania limekua na pia linapokea mabadiliko kila siku suala ambalo pia wasanii wanapaswa kuzingatia ilikukidhi haja za burudani kwa Mashabiki wao.
kwa upande wake anayatazama mabadiliko ya mwanamuziki huyu katika mtazamo chanya na kuongeza kuwa kila mtu anafikra na mtazamo tofauti hivyo kiasi kinahitajika kwa wanasanaa ilikukidhi matakwa ya mashabiki wao,ambao pia wamegawanyika katika matabaka tofauti.


AHOFIA USALAMA WAKE BAADA YA KULALA NA DRAKE

Mwanadada anayejulikana kwa jina almaarufu kama Johni Blaze ambaye ni mnenguaji katika moja ya Kasino maarufu nchini Marekani, amemfungulia mashtaka rapa Drake kwa madai ya kuwa rapa huyo anawatuma watu kumtishia maisha mwanadada huyo suala linalompelekea dada huyo kuishi kwa wasiwasi. mwanadada huyo alifikisha tuhuma hizi polisi akiwa na madai kuwa mwanamuziki Drake anamtumia magenge ya watu kumtisha mwanadada huyo ili asiweze kuvujisha siri ya mahusiano ya mapenzi ya siri yaliyokuwa yakiendelea kati ya mwanadada JOHNI BLAZE na rapa DRAKE kwa hofu ya kuharibu sifa kwa mashabiki zake kwa kushiriki kimahusiano na changudoa. hata ivyo watu wa karibu na mwanamziki DRAKE Walikanusha madai ya mwanadada huyo kushiriki tendo la ndoa na mwanamziki Drake na kuyataja mashitaka na madai ya mrembo huyo kama mbinu chafu anazifanya mwanadada huyo ilikuweza kujipatia umaarufu kupitia jina la mwanamziki DRAKE

HIVI NDIVYO ILIKUWA MAVOCO ALIPOTAKIWA KUSHOOT VIDEO KARIBU NA MNYAMA CHEETAH

Ni baada ya watanzania wengi kupongeza juu ya ubunifu na uzuri wa video mpya ya wimbo wa msanii Richard Mavoco ulioshutiwa huko capetown Afrika ya kusini ambapo ndani ya wimbo huo msanii Richard mavoco anaonekana akiimba karibu kabisa na mnyama wa porini aina ya cheetah, msanii huyo amefunguka juu ya vile alivyopatwa uwoga wakati wa zoezi zima la kupiga picha na cheetah" "Nakumbuka wakati tumefika pale hali ilibadirika ghafla cause mpango ulikuwa ni kwamba Cheetah apigwe shot za peke yake akiwa anatenbea,lakini Adam akabadilisha script akasema Mavoco inabidi uimbe na Cheetah,mwanzo niligoma kabissa lakini kwa ushawishi wa yule mama anayemfuga na Adam ikajikuta nimekubali.

HUZUNI IKIZIDI FURAHA NI MUDA MWAFAKA WA KUVUNJA MAPENZI: JASON DA RULO

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa RNB na POP kutoka nchini Marekani JASON DE RULO ameweka wazi kuwa sababu kuu ya kuvunjika kwa mahusiano kati yake na mwanamziki JORDAN SPARKS ni kukithiri kwa mafarakano kati ya wapenzi hao wawili. JASON alifunguka kuhusiana na kuvunjika kwa mahusiano yao katika mazungumzo na Ryan Seacreth ambapo Jason alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyochochea kukosekana kwa amani ya mahusiano kati ya wawili hao ni pamoja na shinikizo la ndoa kati yao na mwanadada huyo JORDAN SPARK. awali kuvunjika kwa mahusiano kati ya wawili hao kulileta taharuki kubwa hususani ni miongoni mwa mashabiki na watu waliokuwa wakifuatilia mahusiano wanamziki hawa kwani awali haikuwahi kuripotiwa habari yoyote ya mafarakano baina ya wapenzi hawa. Katika mazungumzo na ryan Seacreth De Rulo alikiri kuwa kuvunjika kwa mahusiano hayo haikuwa kwa uzuri lakinhakuna chuki yoyote inayoendelea kati yao kwani wameachana kwa amani njema na sio shari kama ilivyokuwa kwa copules wengine.

JAYZ- AJISOGEZA UGANDA

Rapper na mwanamuziki nguli wa mziki wa hiphop nchini Marekani JAYZ ameripotiwa na chombo cha habari cha THE INSIDER kuwa amefungua tawi la club yake almaarufu kama CLUB 40/40 katika jiji la kampala nchini Uganda. the Insider imeripoti kuwa CLUB 40/40 iliyopo nchini humo itakuwa ni tawi la kwanza kabisa nchini Afrika la CLUB YA 40/40 ambayo kwa sasa imekuwa na umaarufu mkubwa miongoni mwa wasanii na watu maarufu nchini Marekani

Saratani ya shingo ya kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi

SIKILIZA HIPHOPZONE NA FLAVOUR ZA CHAPTER HAPA

SIKILIZA HIPHOPZONE NA FLAVOUR ZA CHAPTER HAPA